Mawakili wa Guantanamo walalamika

Mawakili wa watu watano walioshtakiwa kupanga njama ya mashambulio ya September 11, wamelalamika hadharani kama mahakama ya kijeshi ya Guantanamo Bay ni ya haki kweli.

Haki miliki ya picha AP

Washtakiwa, akiwemo Khalid Sheikh Mohammed, anayeshukiwa kupanga mashambulio ya Septemba 11, na vitendo vengine ya ugaidi, walishtakiwa rasmi Jumamosi.

Mawakili wa washtakiwa wanasema mahakama yanazinga ushahidi kuhusu mateso.

Mawakili wa upande wa washtakiwa huko Guantanamo, ni mchanganyiko wa mawakili wa kijeshi na kiraia, ambao walizungumza na waandishi wa habari kwa pamoja.

Walilalamika juu ya kile walichoeleza kuwa "sheria iliyopangwa" na ambayo "imevikwa pazia la siri"; ambayo walisema inawazuwia kuzusha maswala mahakamani kuhusu yale waliyotendewa washtakiwa wakati wanazuwiliwa na Marekani.

Khalid Sheikh Mohammed alitishiwa mara nyingi kuzamishwa, kwenye magereza ya siri ya CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo.

Wakili wake, David Nevin, alisema: " kila kitu kinafanywa ili kuzuwia kesi hii kuwa ya haki".

Kufuatana na kanuni za mahakama, mawakili piya wanakatazwa kuzungumza na wateja wao kuhusu mateso.