Muingereza Kizimbani Mombasa

Jermaine Grant Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jermaine Grant

Raia wa Uingereza ambaye ni mwislamu na mwenye msimamo mkali amefikishwa katika mahakama moja katika mji wa Mombasa nchini Kenya .

Upande wa mashtaka amesema kua mtuhumiwa anahusishwa na mjane wa mmoja wa walipuaji wa tareh 7 mwezi wa saba mwaka 2007 mjini London.

Mashtaka yanasema kua Jermaine Grant, mwenye umri wa miaka 29, alishirikiana na Samantha Lewthwaite, mjane wa mlipuaji mwingine wa London Jermaine Lindsay anayetafutwa vibaya.

Mashtaka haya yanatokea wakati Grant akitokea kwa mara ya kwanza mbele ya Mahakama katikati ya hali ya taharuki mjini Mombasa.

Mshitakiwa hata hivyo anakanusha madai yote na kuwa alipatikana na vifaa vya kutemgenezea vilipuzi.

Grant -aliyekamatwa mwezi Disemba - tayari anakabiliwa na kosa la kuingia nchini Kenya kinyume cha sheria.

Mwanasheria wa serikali ya Kenya Jacob Ondari anadai kua Grant na Bi. Lewthwaite walishirikiana kutekeleza njama hio.

"inaaminika kua Bi Lewthwaite ndiye mdhamini wa njama yote hii, alisema Bw.Ondari.

Bi. Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 28, anasakwa na serikali ya Kenya na inaaminika anasafiria paspoti bandia. Mume wake alijilipua mwenyewe katika kituo cha treni ya chini ya ardhi mjini London tareh 7 mwezi julai mwaka 2005 akiua watu 26.

Upande wa mashtaka utadai kua mtuhumiwa pamoja na raia watatu wa Kenya, wakipanga njama ya kutumia milipuko walikusudia kuwaua raia.

Kesi hii ilishindwa kuanza mapema jumatano kwa sababu hati za Grant kuhusu uhalifu wake hazikukamilika.