Mapigano yanaendelea Syria

Tume ya UN SYRIA Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Tume ya UN Syria

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mashambulio ya bomu inazidi kuzua masuali juu ya jukumu la waangalizi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Jukumu lao ni kusimamia na kuona kua mapigano yanasimamishwa. Lakini ingawa hilo limetimizwa katika baadhi ya maeneo ukweli ni kwamba mapigano bado hayajamalizika.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano bado yapo

Na hili linazua suali nyeti juu ya umuhimu na uwajibikaji wa tume ya Umoja wa Mataifa.

Imani iliyokuepo ilikua kwamba endapo watatumwa wasimamizi kutoka nje huenda wakasaidia kushawishi wakuu wa serikali kutimiza ahadi zao za kukomesha ghasia.

Lakini tangu mwanzo, kuwepo kwa wasimamizi hawa kulizua suali jipya kuu: Endapo mashambulizi dhidi ya raia yataendelea Je nini kitafuata?

Umoja wa Mataifa utachukua hatua gani zaidi ya hio? Na ni mazingira gani yatafanya Umoja wa Mataifa ukubali kua mpango wake umeshindwa?

Tatizo ni kua hakukuepo mpango mbadala endapo huu utashindwa.

Mpango pekee ambao Jumuia ya kimataifa uliweza kukubaliana kwa sauti moja ni huu wa kutuma wasimamizi. Pamoja na maneno mazuri ya kuvutia ya njia za kupitia kunusuru maisha bila bughdha au njia nyingine za upatanishi, hakuna yeyote aliyetaka kuhusika moja kwa moja na matatzio ya Syria.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makundi yananufaika kwa ghasia

Ingawaje kuhusika kupitia makundi ni njia nyingine. Bila shaka silaha zimekua zikitiririshwa kutoka nje ya nchi. Kukiwa na makundi ndani ya nchi ambayo yanafurahia kuzusha fujo kwa manufaa yao.

Mgogoro wa Syria umeanza kujenga sura ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na Umoja wa Mataifa haujajiweka tayari kutangaza ujumbe wa tume yake umeshindwa kwa sababu hakuna yeyote anayyeweza kujibu suali - Nini kitafanyika sasa.