Rais wa Ugiriki ajaribu kuunda serikali

Rais wa Ugiriki anachukua hatua ya mwisho ya kujaribu kuunda serikali ya dharura ili kuepuka uchaguzi mwengine.

Haki miliki ya picha AP

Atawaita viongozi wa vyama kujaribu kufikia muafaka.

Ugiriki iko kwenye mkwamo, baada ya uchaguzi wa Jumapili iliyopita kushindwa kutoa mshindi.

Viongozi wa vyama vitatu hadi sasa wameshindwa kuunda serikali ya mseto itayopambana na msuko-suko wa kiuchumi wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini Athens anasema haikuelekea kutapatikana ufumbuzi, kwa vile kuna tofauti kubwa baina ya viongozi kuhusu mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuiokoa Ugiriki, na hamasa za wananchi juu ya hatua kali za mpango huo.

Endapo mazungumzo yatakwama itabidi uchaguzi mwengine ufanywe, huku kura za maoni zinaonesha kuwa vyama vinavopinga mbano wa matumizi ya serikali vinaweza kupata viti vya kutosha kuunda serikali.