Vita vya mihadarati vyauma Mexico

Wakuu wa Mexico wamegundua miili iliyokatwakatwa ya watu kama 37, iliyotiwa kwenye mikoba ya plastiki na kutupwa kwenye barabara kuu, karibu na mji wa Monterrey, kaskazini mwa nchi.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Miili hiyo ilikutikana Jumapili alfajiri.

Inaelekea mauaji hayo ndio ya karibu kabisa, katika mfululizo wa mauaji ya kikatili, yaliyohusika na mizozo inayoendelea baina ya magengi yanayouza mihadarati.

Jumatano iliyopita, maiti 18 zilikutikana zimekatwa vichwa na jinsi, karibu na mji wa pili kwa ukubwa nchini Mexico, mji wa Guadalajara.