NATO yapinga kuwaua raia wa Libya

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mashambulio ya NATO Libya

Shirika la kujihami la NATO limepinga ripoti inayolitaka kuchunguza vifo vya raia wa Libya waliouawa katika harakati za jeshi la NATO mwaka jana. Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema raia 72 waliuawa na kutaka NATO kuwajibikia mauaji hayo.

Hata hivyo msemaji wa NATO amesema harakati za jeshi hilo ziliendeshwa kwa uwangalifu mkubwa hususan usalama wa raia.

Ndege za kijeshi kutoka Marekani, Uingereza, na Ufaransa ziliendesha zaidi ya mashambulizi elfu tisa yakilenga kuyumbisha jeshi na utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.Human Rights Watch imesema raia walikufa katika mashambulizi wanane yaliyofanwa na ndege za NATO.

Katukio moja shambulio la bomu liliwaua watu 14 na baadaye watu wengine 18 waliokwenda kuwakoa majeruhi wakaangukiwa na bomu lingine na kufariki papo hapo.

NATO imesema iko tayari kushirikiana na utawala mpya wa Libya katika uchunguzi wa matukio ya mwaka jana.

Hata hivyo shirika hilo limepinga kuwajibikia mauaji hayo kwa sababu hakuna thibitisho kamili dhidi ya mauaji hayo.