Msanii maarufu Donna Summer afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donna Summer afariki dunia katika umri wa miaka 63

Donna Summer, aliyepata umaarufu kwa vibao vya disco kama I Feel Love, Love To Love You Baby na Love's Unkind, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.

Summer alikuwa ni miongoni mwa wasanii mashuhuri sana wa mtindo wa disco aliyewahi kutunukiwa tuzo tano za Grammy kati ya 1978 na 97.

Alishirikiana na Producer Giorgio Moroder katika kuimarisha mtindo wa disco duniani kote.

Alizaliwa akiwa na jina la LaDonna Andre Gaines, alikulia mjini Boston na alianza kuimba katika kwaya ya kanisani.

Alianza kuimba katika tamthilia ya muziki Hair katika miaka ya mwisho ya 1960 nchini Ujerumani ambako hatimaye ndiko alikoamua kuishi.

Rekodi yake ya kwanza aliitoa mwaka 1971 lakini ni ushirikiano wake na msanii wa Kitaliana Moroder ndio uliomletea umaarufu kwa kibao maarufu cha Love to Love You Baby mnamo mwaka 1975.