Mwenge wa Olimpiki wawasili Uingereza

Maelfu ya watu wamejitokeza kutazama mwenge wa Olimpiki ukipita, kuanza safari ya kutembezwa kwa siku 7 sehemu mbali-mbali za Uingereza, kabla ya michezo ya London mwezi wa Julai.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bingwa wa mbio za jahazi, Ben Ainslie, ambaye ameshawahi kushinda medali tatu za dhahabu kwenye Olimpiki, alikuwa wa mwanzo kati ya watu 8,000 wataobeba mwenge huo - kuanzia Land's End, katika jimbo la Cornwall.

Mwenge huo utatembezwa na watoto, watu waliojitolea, pamoja na wanariadha, kabla ya kufikishwa kwenye uwanja wa Olimpiki mjini London, tarehe 27 Julai.