Wasomali watoroka Afgoye

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vita dhidi ya Al Shabaab

Wanajeshi wa muungano wa Afrika na wale wa serikali ya mpito ya Somalia wamesema wameendelea mashambulio yao dhidi ya wapiganaji wa al shabaad na wamekaribia takriban kilomita kumi viungani mwa mji wa afgoye.

Msemaji wa jeshi la pamoja la muungano wa afrika Paddy Ankunda ameiambia BBC kuwa, wamepiga hatua kubwa kukabiliana na wapiganaji hao wa kiislamu wa al shabaab.

Kamanda mmoja wa al shabaab ameuawa kwenye mashambulio hayo yaliyoanza hiyo jana. Ankunda amesema wanajeshi wake watatu walijeruhiwa.

Zaidi wa wakimbizi elfu mia nne ambao walitoroka mapigano mjini mogadishu wanaishi katika mji huo wa afgoye ambao up magharibi mwa mogadishu.

Maelfu ya Wasomali wanendelea kutoka mapigano hayohuku jeshi la Muungano wa Afrika wakisongea karibu na eneo la Afgoye ambalo ni ngome la wapiganaji wa Al Shabaab, karibu na mji mkuu Mogadishu.

Wanajeshi hao wamesongea hadi kilomita kumi karibu na mji huo unaodhibitiwa na al-Shabab. Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa muungano wa AU.

Wenyeji walioko katika eneo la mpakani kati ya mji mkuu na Mji wa Afgoye, wameambia BBC kuwa watu wengi wametorokea Mogadishu au maeneo yanayozingira mji huo.