Jeshi la Syria na upinzani hatiani

Mlipuko huko Hamas Haki miliki ya picha s
Image caption Mlipuko huko Hamas

Ripoti iliyoidhinishwa na kuchapishwa na tume ya Umoja wa Mataifa imesema kua vikosi vya usalama nchini Syria ndivyo vinavyowajibika na vitendo vya uvunjanji wa haki za binadamu vilivyofanyika kuanzia mwezi March mwaka huu.

Ripoti hio inataja pia ujanja uliotumiwa na upinzani ushahidi ukionyesha kua askari waliotekwa wakinyanyaswa kabla ya kuuawa.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema kua mzozo huo umegeuka na kua zaidi wa kijeshi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ghasia Syria

Katibu mkuu wa Umoja huo Ban Ki-Moon anasema kua kwa uchache ni watu 10,000 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa vuguvugu la mapinduzi la mwezi Machi mwaka 2011.

Katika taarifa yake ya hivi karibuni, ikiangaz vitendo vya kihalifu kati ya mwezi Machi, Aprili na sehemu ya mwezi meyi, tume hio iliyotumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, iliandika juu ya matukio ya unyanyasaji na hukumu za haraka za mauaji yaliyofanywa na pande zote zinazohusika na mgogoro wa Syria, yaani Jeshi la Syria na upinzani.

Mengi ya maovu yaliyokiuka haki za binadamu katika taarifa ya tume hio ni uovu uliotendwa na jeshi la Syria pamoja na vikosi vya usalama wa taifa kama sehemu ya operesheni za kijeshi katika maeneo yanayoshukiwa kuunga mkono makundi yanayoipinga serikali.

"jeshi lilitumia ujanja wa aina mbalimbali wa kijeshi ikiwa ni pamoja na kutumia makombora mazito katika kushambulia maeneo yanayokaliwa na raia.