Darubini kubwa duniani kuwa Afrika

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Darubini

Afrika Kusini, Australia na New Zealand zimeafikiana kujenga darubini kubwa zaidi duniani.

Haya yametangazwa katika mkutano kati ya nchi tatu mjini Capetown.Darubini zote zitatumika katika kuimarisha teknolojia ya fanaki.

Ni darubini ambazo zitasaidia kufahamu maisha katika sayari nyingine. Mradi huu unanuia kujenga darubini zitakazochukua upana wa viwanja vya mpira.

Afrika Kusini na Australia zilituma maombi tofauti, na inaonekana hakutakuwa mshindi wa moja kwa moja ndipo zikaamua kushirikiana pamoja.