Mtumishi wa Papa Benedict akamatwa

Polisi wa Vatikani wamemshtaki rasmi mtumishi wa Papa Benedict, katika kesi inayohusu wizi wa nyaraka za siri.

Haki miliki ya picha Reuters

Paolo Gabriele - ambaye akitumika kwenye fleti ya papa - amezuwiliwa Vatikani, na ameruhusiwa kuonana na mawakili wawili.

Wakuu wanachunguza vipi, katika miezi ya karibuni, magazeti ya Utaliana yalipata nyaraka ambazo zinaeleza mashindano kati ya wakuu wa kanisa - kisa ambacho kimeanza kuitwa 'Vatileaks'.

Inaarifiwa kuwa Papa Benedict ameshangazwa na kusikitishwa kuwa mtumishi wake mmoja amekamatwa.

Mkuu wa Benki ya Vatikani alitolewa kazini Alkhamisi, kutokana na kashfa hiyo.