Wamorocco wataka ahadi zitimizwe

Maelfu ya watu wameshiriki kwenye maandamano dhidi ya serikali katika mji mkubwa kabisa wa Morocco, Casablanca.

Haki miliki ya picha Reuters

Vyama vya wafanyakazi vimeandaa maandamano hayo - ambayo yanafikiriwa kuwa ndio makubwa kabisa tangu serikali mpya kushika madaraka mwezi wa Januari.

Wanawalaumu wakuu kuwa hawakutimiza mabadiliko waliyoahidi wakati wa maandamano ya mwamko wa mwaka jana.

Serikali ya Kiislamu ya wastani ilichaguliwa mwezi wa Novemba, baada ya Mfalme Mohammed kuchukua hatua kupunguza madaraka yake.