Urussi yashutumu Syria kushambulia raia

Yevgeny Lavrov Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Yevgeny Lavrov wa Urussi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa yake kulaani hatua ya Serikali ya Syria kwa kufanya mashambulizi kwa kutumia Vifaru vya Kijeshi na Makombora dhidi ya Mji wa Houla.

Kauli ya Urussi ikishutumu matukio nchini Syria kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kumezusha suali kama ni mabadiliko katika msimamo wa nchi hiyo kuhusu Syria.

Na je ikiwa ni hivyo, Rais Basher al Assad atakabiliwa na shinikizo zaidi ? Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urussi Sergei Lavrov alionekana kuiwekea Syria hali ngumu lakini alidokeza kua kwa Urussi haidhuru ni nani aliye madarakani nchini Syria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mauwaji ya Houla

Hadhi ya Taifa lazima iheshimiwe, alisema lakini juu ya yote Urussi inataka kuona ghasia zikikomeshwa nchini humo.

Uchina pia iliunga mkono Taarifa ya Umoja wa Mataifa. Lakini ni Urussi ambayo mchango wake juu ya sakata hii ni muhimu. Nchi hio ina uhusiano wa karibu wa kisiasa,kiuchumi na kijeshi na utawala wa Assad. Wakati Marekani ikizidi kushinikiza kuwepo na mageuzi kama yaliyofanyika huko Yemen, Urussi ambayo ina uelewa wa ndani wa Syria itakua muhimu mno.

Hata hivyo umuhimu wake uzizishwe chumvi. Mpango wa Annan, ambao Urussi ilikubaliana nao, wa kusitisha mapigano na kuanza mchakato wa kisiasa unaonekana kama ulioshindwa kutekeleza.

Wasimamizi wa Umoja wa Mataifa walioko Syria wanathiniobitisha kile wengi walichokitarajia- kua ghasia zitaendelea. Tatizo ni kwamba Umoja wa Mataifa pamoja na jumuia ya kimataifa haukuwa na mpango mbadala wa huo wa Annan.

Hakuna tamaa ya nguvu ya kijeshi kutumika kwenye hatua hii. Rais Assad anaambiwa kina ubaga angatuke madaraka na hataki kufanya hivyo. Huku umwagaji damu ukiendelea na kile juhudi kushindwa uwezekano wa nchi hio kuingia kua vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe ni mkubwa. Na ishara zipo kua Mataifa ya Ghuba yanayodhani kua njia pekee ni kuwapa silaha upinzani wa Syria wanazidisha juhudi zao kwa sasa.V