Brotherhood kujumuisha wote,Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mohammed Mursi

Mgombea wa Urais mrengo wa Muslim Brotherhood nchini Misri Mohammed Mursi, amesema kwamba atajumuisha makundi yote ya kisiasa katika serikali endapo atashinda duru ya pili ya Urais.

Mursi ameahidi haya katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema atahakikisha kuwepo kwa uwakilishi wa wanawake na vijana.Kiongozi huyo wa chama cha Freedom and Justice amesema kwamba nia yake ni kuondoa utawala wa kiimla na kuweka msingi thabiti katika taasisi za uwongozi.

Matamshi ya Bw. Mursi yanajiri wakati afisi za hasimu wake Ahmed Shafiq zimeteketezwa na watu wanaodhaniwa wafuasi wafuasi wa makundi ya kiisilamu.

Watu wanne wamekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.Awali maelfu ya raia waliandamana nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi kufuatia matokeo ya raundi ya kwanza ambapo Bw Mursi alishinda kwa asilimia 24.3 dhidi ya Bw Shafiq aliyepata asili mia 23.3 ya kura.