Sherehe za Diamond Jubilee zaanza

Sherehe za siku nne zinaanza Jumaosi Uingereza, kuadhimisha miaka 60 ya tangu Malkia Elizabeth kuvikwa taji - sherehe za Diamond Jubilee.

Haki miliki ya picha AFP

Jumamosi, mizinga 41 ilisikika mjini London siku alipochukua umalkia rasmi.

Malkia anahudhuria mashindano ya mbio za farasi - Epsom Derby.

Na Jumapili mlolongo wa meli na mashua 1000 zitamsindikiza kwenye Mto Thames.

Karabai zaidi ya 4000 zitawashwa sehemu mbali-mbali za dunia, kusherehekea Malkia Elizabeth kutimiza miaka 60 kwenye kiti cha ufalme.