Tuhuma nyengine za rushwa Afrika Kusini

Shirika linaloendesha treni za kasi za Afrika Kusini, Gautrain, limekanusha taarifa za magazeti zinazotuhumu kuwa kandarasi ilipatikana baada ya kulipa dola milioni-35.

Gazeti moja la Afrika Kusini limetoa taarifa inayosema kuwa kamisheni ililipwa na kampuni ya Canada iliyotengeneza treni hizo, Bombardier, kwa mfanya biashara wa Tunisia na muuza silaha, Youssef Zarrouk.

Inaarifiwa kuwa kampuni husika na mfanya biashara huyo, wamethibitisha kuwa fedha hizo zililipwa, lakini walisema hayo ni malipo ya wakala.

Treni za Gautrain zilikusudiwa kusafirisha abiria kutoka uwanja wa ndege wa Johannesburg hadi kati ya mji huo, na mji wa Pretoria.

Umoja wa vyama vya upinzani, Democratic Alliance, umetaka kufanywe uchunguzi juu ya kandarasi hiyo.