Wakimbizi wengi waingia Sudan Kusini

Shirika la kimataifa la msaada wa matibabu la Medecins sans Frontieres, linasema kwamba idadi ya wakimbizi wanaowasili Sudan Kusini, wanaokimbia mapigano ya kaskazini, imeongezeka sana.

Haki miliki ya picha AFP

Watu baina ya 2000 na 4000 wanavuka kila siku kutoka jimbo la Blue Nile, kukimbia mapigano baina ya serikali ya Khartoum na wapiganaji.

MSF inasema watoto wengi wanatapia mlo sana, baada ya kutembea kwa majuma mawili.

Wakimbizi wanasema baadhi ya wazee na wagonjwa walidhoofika sana, na walifariki njiani.

Watu zaidi ya 100,000 sasa wanaishi kwenye makambi karibu na mpaka.