Hukumu ya Mubarak yakatiwa rufaa

Afisa wa mashtaka wa Misri, amekata rufaa kupinga hukumu ambayo ilifuta mashtaka ya rushwa dhidi ya Rais Hosni Mubarak na watoto wake wawili wa kiume, na kufuta piya mashtaka dhidi ya wakuu wa polisi, kuwa walishiriki kwenye mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia za mwaka jana.

Haki miliki ya picha AFP

Wakuu wanasema afisa wa mashtaka alitoa amri kuwa makamanda sita wa polisi hawana ruhusa ya kusafiri hadi rufaa ifikishwe mahakamani.

Hukumu iliyotolewa Jumamosi juu ya rais wa zamani, Mubarak, ilizusha maandamano makubwa mjini Cairo na miji mengine siku ya Jumamosi.