Hali ya mume wa Malkia inaimarika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Malkia Elizabeth na Mumewe Phillip

Hali ya mume wa Malkia wa Uingereza "imeimarika" lakini anatarajiwa kuwepo hospitali katika siku chache zijazo, taarifa kutoka kwa Kasri ya Buckingham imesema.

Prince Philip mwenye umri wa miaka 90, amekuwa hospitali kwa siku mbili akitibiwa matatizo ya kibofu cha mkojo, na alikosa sherehe za mwisho za kuadhimisha miaka sitini ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili.

Msemaji wa Kasri ya Buckingham anasema Prince Philip "yuko katika hali nzuri".

Prince Philip alipelekwa hospitali siku ya Jumatatu, saa chache kabla ya tamasha la muziki lililofanyika nje ya Kasri ya Buckingham.

Anatibiwa katika hospitali ya Mfalme Edward wa saba katikati mwa London.

Msemaji wa kasri alisema: " Anaendelea na matibabu na anapewa dawa kwa sasa.

" Anatarajiwa kubaki hospitali katika siku chache zijazo. Yuko katika hali nzuri."

Siku ya Jumanne, mwanae mdogo wa kiume wa Malkia, alisema babake "yuko vizuri".