Miili ya watu 14 imepatikana Mexico

Milli ya watu iliyokatakatwa nchini Mexico Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Milli ya watu iliyokatakatwa nchini Mexico

Serikali ya Mexico imesema kuwa imapata miili ya watu 14 ambayo imekatakatwa ndani ya lori iliokuwa imeegezwa nje ya ofisi ya meya wa mji wa Ciudad Mante, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa ujumbe ulioandikwa na kundi moja la kigaidi limepatikana ndani ya blanketi iliyotumika kufunika miili ya watu hao.

Miongoni mwa walioauawa ni wanaume kumi na mmoja na wanawake watatu.

Mauaji hayo yametokea siku moja baada mgombea anayeongoza katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha urais, Enrique Pena Nieto, kuzuru jimbo hilo na kuhaidi kuwa atapunguza viwango vya mauaji ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa taifa hilo.

Tangu mwaka wa 2006 Mexico imeshuhudia misururu ya ghasia zinazohusiana na ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya rais wa nchi hiyo Felipe Calderon, kutoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kuyasaka makundi ya walanguzi wa mihadarati.