Hali ya Syria yatia wasiwasi Urusi

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema Urusi inazidi kuingiwa na wasiwasi kuhusu hali nchini Syria, lakini haitaruhusu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha utumizi wa nguvu kutafuta ufumbuzi.

Haki miliki ya picha Reuters

Bwana Lavrov alisema matukio nchini Syria yanashtusha.

Lakini alisema Urusi bado inaamini kuwa mataifa ya nje yakiingia Syria kwa nguvu kumaliza msukosuko huo, zinaweza kuleta mtafaruku katika eneo zima, na matokeo kuwa mabaya sana.