Waziri mdogo wa Marekani afika Mogadishu

Naibu Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, anayeshughulika na maswala ya Afrika, Johnnie Carson, amewasili mjini Mogadishu, Somalia.

Haki miliki ya picha AFP

Miaka mingi imepita tangu afisa wa Marekani wa daraja kama hiyo, kuzuru mji huo.

Taarifa zinaeleza kuwa Bwana Carson anafanya mazungumzo na wakuu wa serikali ya Somalia, pamoja na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.

Mwezi wa Disemba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alizuru Mogadishu, ambayo ilionekana kama ishara kuwa watu wana imani na usalama mjini humo.

Wapiganaji wa Al-Shabaab walitimuliwa kutoka mji huo mwaka jana.