Duru ya pili ya Uchaguzi Ugiriki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchaguzi Ugiriki

Vyama vya siasa nchini Ugiriki viko katika hatua za mwisho kunadi sera na kuomba kura kabla ya uchaguzi wa marudio siku ya Jumapili.

Uchaguzi huo unaolezwa kuwa muhimu kwa nchi hiyo inayoandamwa na madeni pamoja na mustakabali wa nchi hiyo katika sarafu moja ya Euro.

Chama cha kihafidhina cha New Democracy ambacho kinaunga mkono mpango wa kukopa fedha kunusuru uchumi kiliongoza katika uchaguzi uliopita, kinafanya mkutano mkubwa wa mwisho wa kampeni.

Chama Syriza kinachopinga mpango kukopa fedha kuokoa uchumi ambacho kilishika nafasi ya mwezi Mei, chenyewe kilifanya mkutano wake wa hadhara katika mji Athens siku ya Alhamisi.

Kura za maoni ambazo sio rasmi zinaonyesha huenda vyama vinavyopinga mpango wa kukopa fedha ili kuokoa uchumi vikashindwa.

Chini ya sheria ya uchaguzi nchini Ugiriki ni marufuku kuendesha kura rasmi ya maoni wiki mbili kabla ya uchaguzi.

Tayari hatua mbili za kimataifa za kunusuru uchumi umechukuliwa kwa ajili ya Ugiriki wenye thamani ya euro 110bilioni au dola bilioni 138 za kimarekani mwaka 2010, kisha kufuatilia mpango mwingine wa mwaka jana wenye thamani ya euro 130bilioni

Wakati vyama saba vikuu ya kisiasa vikipinga mpango wa kuokoa uchumi ni chama kimoja tu cha kikomunisti kinataka nchi hiyo kuachana na umoja wa Ulaya.

Ujerumani, ambayo ina nguvu zaidi kiuchumi katika ukanda wa euro , anasisitiza Ugiriki, kama nchi nyingine wanachama wa umoja wa ulaya lazima kuchukua hatua ya kubana matumizi..