Uonevu katika idara ya uhamiaji Uingereza

Image caption Afisaa wa uhamiaji Uingereza

Maafisa wa idara ya uhamiaji ya Uingereza, wanaotayarisha visa za watu kutoka barani Afrika, huwa na uonevu na huwanyima raia wa kiafrika wanaotafuta visa kuingia nchini Uingereza.

Madai haya yako kwenye ripoti iliyotolewa na shirika moja binafsi kuhusu utaratibu wa idara ya uhamiaji ya Uingereza.

Inspekta mkuu wa idara ya uhamiaji ya Uingereza Bwana John VINE amesema kuwa idadi kubwa ya waombaji wa Visa za uingereza hukataliwa kimakosa.

Idara hiyo imesema imechukulia ripoti hiyo kwa uzitio na inatazamia kubadilisha utaratibu wake.

Amsema sababu kubwa sio makosa yanayotokana na waombaji wenyewe bali nikutokana na maafisa wanaoshughulika na maombi hayo.

Bwana John Vine anasema mara nyingi maombi hukataliwa kwa kukosekana stakabadhi ambazo hapo awali muombaji hakuambiwa zinatakikana.

Afisa huyoa nasema hali hii imeaharibu sifa za uingereza na kuwafanya baadhi ya watu waaamini kwamba kuna ubaguzi fyulani unaofanywa.

Japo uchunguzi huo ulifanywa katika nchi za Kenya, Afrika kusini na Nigeria lakini ripoti hiyo inasema uonevu huo katika utoaji wa Visa umesambaa katika nchi nyingi barani afrika.

Katika ripoti yake Inspekta huyo mkuu huyo wa idara ya uhamiaji amesema kwamba imegyundulika kuwa kuna watu kadhaa hasa kutoka Nigeria waliopewa visa ya Uingereza ya kudumu .

Kutokana na ulegevu huo sasa kumependekezwa kuwa maafisa wote katika idara hiyo ya uhamiaji ya uingereza nimuhimu wapewe mafunzo upya.