Wakuu wa Misri wasimamisha bunge

Afisa wa ngazi ya juu wa bunge la Misri ameiambia BBC kua amepokea barua kutoka baraza la kijeshi linalotawala Misri kua limeahirisha bunge.

Hii itakua mara ya kwanza kwa baraza la kijeshi kutangaza rasmi kuahirisha bunge hilo.

Haki miliki ya picha
Image caption Uchaguzi Misri

Habari hizi zinatokea siku ambapo raia wa Misri wamekua wakipiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo tangu Hosni Mubarak alazimishwe kungatuka madarakani mwaka uliopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Moslem Brotherhood

Wagombea wanaopigiwa kura ni aliyekua Waziri Mkuu wa Hosni Mubarak, Ahmed Shafiq na MOHAMED Morsi wa Muslim Brotherhood.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo amesema kua wapiga kura hawakujitokeza kwa wingi kama kawaida, na kwamba vijana wengi wa Kimisri wanaonekana wamekatishwa tamaa na upigaji kura.

Wakati huo huo kuna habari za mapigano kwenye vituo vya kupigia kura katika baadhi ya vituo kufuatia tetesi kwamba watu wanapewa kalamu zenye wino unaotoweka mda mfupi baada ya kuandika.