Prince Nayef wa Saudi Arabia afariki

Taarifa imetangazwa nchini Saudia Arabia ya kifo cha Prince Nayef bin Abdulaziz al-Saud, ambaye akitarajiwa kurithi ufalme.

Haki miliki ya picha

Qasri ya Saudi Arabia ilisema alifariki hospitali katika nchi za nje.

Mwezi wa May prince huyo alikwenda Uswiswi kwa matibabu.

Prince Nayef aikuwa waziri wa mambo ya ndani wa Saudia Arabia tangu mwaka wa 1975, na mwezi Oktoba mwaka jana, akiwa na umri wa miaka 78, aliteuliwa kuwa ndie atayemrithi mfalme wa sasa, Mfalme Abdullah.

Taarifa ilieleza kuwa atazikwa Jumapili mjini Makka.