Mji wa Afgoye, Somalia, washambuliwa

Mshambuliaji wa kujitolea mhanga amevurumisha gari lilojaa mabomu dhidi ya lango la kituo cha serikali ya Somalia, katika mji wa Afgoye.

Haki miliki ya picha AFP

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab alisema mmoja wao alifanya shambulio hilo.

Wanajeshi wa serikali na wa Umoja wa Afrika, AU, waliukomboa mji wa Afgoye kutoka kwa al-Shabaab mwezi uliopita.

Afgoye iko kama kilomita 30 nje ya Mogadishu katika barabara inayounganisha mji huo na maeneo ya kusini mwa Somalia yanayodhibitiwa na wapiganaji.