Suu Kyi atoa hotuba ya Nobel

Mwanaharakati wa demokrasi nchini Burma, Aung San Suu Kyi, hatimae ametoa hotuba yake ya Nobel, miaka 21 baada ya kutunukiwa tuzo ya amani, ambayo hakuweza kuipokea rasmi wakati huo.

Alisema tuzo hiyo iliufungua moyo wake, na kumfanya ahisi kuwa yuko pamoja na ulimwengu ingawa alikuwa kifungoni.

Aung San Suu Kyi alisema tuzo hiyo piya ilihakikisha kuwa juhudi za kupigania demokrasi na haki za kibinaadamu nchini Burma na dunia nzima, hazikusahauliwa.

Alishangiliwa aliposema kuwa wafungwa wote wa kisiasa waachiliwe huru.

Akizungumza baada ya kuonana na waziri mkuu wa Norway, mwanasiasa huyo alitoa wito wageni wawekeze zaidi nchini Burma wakati nchi hiyo inafanya mabadiliko.