BBC yazindua kipindi kipya kuhusu Afrika

Image caption Komla Dumor na Morgan Tsvangirai waziri mkuu wa Zimbabwe

Leo hii BBC imezindua kipindi cha televisheni cha kiingereza "Focus on Afrika" kwenye Televisheni ya BBC World News.

Kipindi hicho kitaileta Dunia Barani Afrika na kitaangazia bara la Afrika na taarifa za Afrika nazo kujilikana Duniani kote.

Focus on Afrika kitatangazwa Jumatatu hadi Ijumaa mnamo saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Mashariki au mija na nusu kwa saa za afrika ya kati, watangazaji wake wakiwa Komla Dumor.

Afrika ni soko kuu la habari za dunia hii ikiwa ni robo ya jumla ya wasikilizaji wa BBC.

Kitu muhimu ni kuwaelezeaa wasikilizaji wa barani Afrika taarifa ambazo zina maana kwao na kipindi hiki kitafanya hivyo , kui-elezeea taarifa kwa watu wa barani Afrika.

Utafiti unaonyesha kuwa mashabiki wa Afrika wanatutaka kuwafahamisha Taarifa za Dunia zenye maana na pia Taarfia kuwa za Baranai Afrka kwenyewe, utamaduni biashara na michezo.

BBC inatumai kupata watazamaji milioni tisa kila wiki ili na kuongeza idadi ya mashabiki wa BBC ikijumulisha wale wa redio ambao idadi yao kwa sasa ni milioni sabini na saba kila wiki,.

Ripoti zake zitakuwa zitokea ofisi zake kubwa mjini Nairobi, Abuja, Johannesburg na Dakar.