Liberia yarudisha wapiganaji Ivory Coast

Serikali ya Liberia imewarudisha Ivory Coast wapiganaji 41.

Haki miliki ya picha Reuters

Wanaume hao walikamatwa wakiwa na silaha na risasi mwezi wa Aprili na kikosi cha Umoja wa Mataifa, walipokuwa wakijaribu kuingia Ivory Coast.

Inadaiwa kuwa wapiganaji hao ni wafuasi wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, ambaye sasa anazuwiliwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa.

Katika mwaka uliopita, mashambulio kadha yamefanywa Ivory Coast kutoka Liberia, ambapo watu kama 60 wameuwawa.

Wananchi wa Ivory Coast kama 70,000 bado wako Liberia, baada ya mtafaruku uliofuatia ghasia za uchaguzi wa mwaka wa 2010, ambapo Rais Alassane Ouattara alishinda.