Ndege ya Uturuki iliingia anga ya Syria

Serikali ya Uturuki inafikiri kuwa ndege yake moja ya kijeshi iliyodunguliwa na Syria Ijumaa, pengine iliingia katika anga ya Syria.

Haki miliki ya picha Reuters

Rais Abdullah Gul, aliliambia shirika la habari la Uturuki, Anatolia, kwamba ni kawaida kwa ndege za kijeshi kuvuka mipaka ya nchi, zinaposafiri kwa kasi.

Bwana Gul alisema serikali yake inawasiliana na Syria kuhusu tukio hilo.

Majeshi ya wanamaji ya nchi zote mbili yanafanya msako wa pamoja kuwatafuta marubani wa ndege hiyo.

Uturuki ilimundosha balozi wake nchini Syria mwezi wa March baada ya ghasia kuzidi nchini humo, lakini Bwana Gul alisema hiyo haizuwii serikali yake kuwasiliana na serikali ya mjini Damascus.