Syria ilidungua ndege bila ya onyo

Uturuki inasema kuwa ndege yake ya kijeshi iliyotoweka Ijumaa, ilikuwa juu ya bahari ya kimataifa, wakati Syria ilipoidungua bila ya onyo.

Haki miliki ya picha AFP

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, alisema ndege hiyo iliiingia kwenye anga ya Syria, lakini haraka iliondoka.

Bwana Davutoglu alishikilia kuwa ndege hiyo haikuwa ikifanya baya.

Syria inasema ndege hiyo ilikuwa karibu na mwambao wake.

Waziri Mkuu wa Uturuki anakutana na viongozi wa vyama vyengine bungeni baadae hii leo, kuamua hatua gani ya kuchukua dhidi ya Syria.

Uturuki imewasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mataifa matano yenye uanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.