Waziri Mkuu wa Hong Kong atawazwa

Rais Hu Jintao wa Uchina ameadhimisha miaka 15 tangu Hong Kong kurejeshewa Uchina, kwa kuahidi kuwa Hong Kong ibaki na uhuru wake wa kadiri fulani.

Kwa wakati wote huo, koloni hiyo ya zamani ya Uingereza, imekuwa ikiendesha shughuli zake wenyewe, chini ya utawala wa Uchina katika sera inayoitwa - taifa moja lenye mifumo miwili ya siasa.

Katika sherehe ya kuapishwa kwa waziri mkuu mpya wa Hong Kong, C.Y. Leung, Rais Hu alisema, Hong Kong imetoa mchango mkubwa katika mabadiliko na marekibisho ya kisasa katika Uchina bara.