Timbuktu ya kale yaendelea kubomolewa

Wapiganaji wa Kiislamu kwenye mji wa kale wa Mali, Timbuktu, wanabomowa makaburi ya mashekhe wa zamani kwa siku ya pili.

Haki miliki ya picha AFP

Baada ya kuangamiza makaburi matatu jana, sasa wanabomowa mengine mane kwa majembe na patasi.

Timbuktu ni mji unaotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa, kuwa mji wa kuhifadhiwa, na inaarifiwa wenyeji wanaangalia kwa hamasa, hawawezi kufanya kitu, wakati historia yao inaangamizwa.

Wapiganaji hao wa kundi la Ansar Dine, wanadai kuwa makaburi hayo yanakwenda kinyume na Uislamu.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na utamaduni, UNESCO, limesema uharibifu huo unasikitisha, na limewataka wapiganaji hao wasite kufanya hivo.