Mgombea wa upinzani anaongoza Mexico

Raia Mexico akipiga kura Haki miliki ya picha Getty
Image caption Raia Mexico akipiga kura

Matokeo ya kura ya maoni ya mwisho nchini Mexico, yamebainisha kuwa kiongozi wa upinzani Enrique Pena Niet'o anaongoza.

Ikiwa Bwana Niet'o atashinda uchaguzi huo, chama cha PRI ambacho kilikuwa uongozini kwa miongo saba kitarejea tena mamlakani.

Mgombea wake, Niet'o anaongoza katika uchaguzi wa Urais.

Viti 500 katika bunge la congress pia vinawaniwa katika uchaguzi huo mkuu.

Maelfu ya maafisa wa polisi na wanajeshi wanashika doria katika vituo vyote vya kupigia kura ili kuzuia walanguzi wa mihadarati kuhujumu zoezi hilo.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, mgombea wa chama cha PRD kinachoongozwa na Andres Manuel Lopez Obrador kinashikilia nafasi ya pili.

Mgombea wa chama tawala cha PAN naye anashikilia nafasi ya tatu.

Katika kinyanganyiro cha umeya wa mji mkuu, mgombea wa chama cha mrengo wa kushoto Mioguel, Angel Mancera anaongoza.