Bob Diamond wa Barclays ajiuzulu

Haki miliki ya picha s
Image caption Bob Diamond

Aliyekuwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays, moja ya benki kubwa zaidi nchini Uingereza, atahojiwa na kamati maalum ya bunge hii leo.

Bwana Bob Diamond, aliyejiuzulu jana anatarajiwa kuhojiwa kuhisiana na sakata ya kuongezwa kwa viwango vya riba iliyomfanya ajiuzulu

Diamond, alijiuzulu jana baada ya benki ya Barclays kushutumiwa vikali kwa hujuma za kuongeza viwango vya riba kinyume cha sheria.

Benki hiyo imepigwa faini mabilioni ya dola kufuatia kashfa hiyo.

Akizungumza na BBC mjumbe wa kamati ambayo itamhoji Bwana Diamond hii leo, John Mann amesema hatarajii kuwa bwana Diamond akubali kuwajibika na sakata hiyo