Ujenzi wa bwawa umeanza tena Lao

Ramani ya Laos
Image caption Ramani ya Laos

Wanaharakati wa mazingira wanasema wanasema serikali ya Laos imeanza ujenzi wa mradi wa bwawa la maji katika mto Mekong, ambao umekuwa ukipingwa vikalu na mataifa jirani.

Waandishi wa habari wa BBC, hawakuruhusiwa kuzuru bwala hilo katika eneo la Xayaburi, lakini kwa mujibu wa picha za video zilizonakiliwa na shirika la Kimataifa linalohusika na mikakati ya kuhifadhi mito la International Rivers, mradi huo wa ujenzi umeonekana kuanza.

Serikali ya Laos imesema kazi hiyo inayoendelea ni matayarisho na hakuna uamuzi wowote ambao umeafikiwa ikiwa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la maji utaendelea au la.

Serikali ya Cambodia na Vietman pamoja na mashirika mengine ya kutetea mazingira, wanataka utafiti wa athari za mradi huo kwa mazingira, viwango vya samaki na viumbe vingine katika mto huo kufanyika kabla ya mradi huo kuruhusiwa kuendelea.