Korea Kusini kuvua Nyangumi

Uvuvi wa Nyangumi nchini Korea Kusini Haki miliki ya picha PA
Image caption Uvuvi wa Nyangumi nchini Korea Kusini

Korea Kusini imetangaza kuwa inataka kuanza uwindaji wa nyangumi chini ya sheria inayoruhusu uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya utafiti wa kisayansi, kama vile serikali ya Japan inavyofanya kwa sasa.

Serikali ya Korea Kusini, ilifichua hayo wakati wa mkutano wa kimataifa wa baraza linalosimamia na kulinda maslahi ya nyangumi nchini Panama, ambako walikuwa wakiwasilisha mipango yao kwa kamati ya sayansi ili kuchunguzwa.

Nyangumi hao watawindwa karibu na pwani ya Korea lakini haijulikana ni wangapi.

Uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya biashara imepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa, lakini uwindaji wa nyangumi kwa minajili ya utafiti unaruhusiwa, hata kama nyama yake italiwa baadaye.

Korea ina historia ya ulaji wa nyama ya nyangumi kuliko eneo lolote ulimwenguni, na inakisiwa kuwa urauibu huo ulianza takriban miaka elfu nane iliyopita.