Wanafunzi wakamatwa Burma

Wanaharakati wanaotetea demokrasi nchini Burma, wanasema kuwa wanafunzi zaidi ya 20 wamekamatwa, katika hatua kubwa kabisa ya kuzima upinzani, tangu mabadiliko ya siasa kuanza nchini hum, mwaka jana.

Walikamatwa kabla ya maadhimisho ya hatua kali zilizochukuliwa dhidi ya wanafunzi miaka 50 iliyopita.

Watu kama 300 wamekusanyika mjini Rangoon kuadhimisha tukio hilo, ingawa wenzao wamekamatwa, na askari kanzu kuwepo.

Mwandishi wa BBC anasema ikiwa wanafunzi hao hawakufunguliwa haraka, basi kutazuka maswala kama kweli serikali inakusudia kuleta mabadiliko.