Garcia Marquez aanza kupoteza akili

Kaka wa mwandishi wa riwaya wa Colombia, Gabriel Garcia Marquez, amethibitisha kuwa mwandishi huyo aliyewahi kutunzwa tuzo ya Nobel, anapotewa na akili.

Haki miliki ya picha AP

Jaime Garcia Marquez aliwaambia wanafunzi katika mji wa Cartagena, kwamba mwandishi huyo, mwenye umri wa miaka 85, anaanza kupoteza kumbu-kumbu na hivi sasa hatungi vitabu.

Lakini alisiitiza kuwa nduguye yuko katika hali njema kimwili.

Riwaya maarufu ya Gabriel Garcia Marquez, One Hundred Years of Solitude, inaanza na hadithi ya familia isiyoweza kumuangalia babu yao, anayeaanza kupoteza akili uzeeni.