Afghanistan yapata msaada mkubwa

Mkutano wa mataifa yanayoifadhili Afghanistan, uliofanywa mjini Tokyo, Japani, umeahidi kuipa nchi hiyo dola bilioni 16, ili kuisaidia baada ya majeshi ya kigeni kuondoka mwaka wa 2014.

Haki miliki ya picha BBCPashto.com

Lakini wajumbe wa nchi hizo zaidi ya 70, wameitaka Afghanistan ipambane na ulaji rushwa.

Akihutubia wajumbe hapo awali, Rais Hamid Karzai alisema, juhudi za kuleta amani, utulivu, na kuijenga nchi, hazitafanikiwa bila ya msaada wa mataifa mengine.

Aliahidi kupambana na rushwa:

"Mabibi na mabwana, natambua kuwa ushirikiano wetu utafanikiwa iwapo sisi tutawajibika, na kuthibitisha uongozi wetu ni sawa, ili kuhakikisha kuwa fedha za walipa kodi wenu mtazotupa, zinatumika kuleta manufaa na kwa njia wazi."