Wafungwa Malawi watimka

Wafungwa kwenye gereza moja ya Malawi wamefanya ghasia kupinga msamaha waliopewa baadhi ya wafungwa wenzao, ambao wanaona haukuwa wa haki.

Haki miliki ya picha AFP

Rais Joyce Banda, siku ya Ijumaa aliwasamehe wafungwa karibu 400, lakini siyo wale waliofungwa kwa sababu ya mauaji au ubakaji.

Wafungwa katika gereza ya Zomba, mashariki mwa nchi, walitoroka kwenye seli zao na kuwabughudhi wasimamizi, wakisema wafungwa wawili waliosamehewa ni wahalifu wa mauaji na ubakaji.

Bibi Banda alisema wabakaji wanafaa kufa jela, hasa wale waliowabaka watoto.

Ubakaji wa aina hiyo unatokea mara kadha Malawi, kwa sababu kuna wanaoamini kuwa kufanya mapenzi na msichana bikira kunaleta mali na kunatibu HIV na UKIMWI.