Misaada yatakikana kuokoa Dadaab

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya wakimbizi katika kambi ya Dadaab, Kenya

Mashirika ya kuto misaada katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani , Dadaab yamesema yamepungukiwa na pesa.

Makundi hayo yameonya kuwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa basi hali ya maisha ya maelfu ya wakimbizi yatakuwa hatarini.

Mashirika manane yakiwemo ,Oxfam na Save the Children, yamesema kunaupungufu wa dola milioni 25m na kwamba kuna mahitaji makubwa zaidi.

Idadi ya wakimbizi katika kambi hiyo ya Dadaab ambayo iko karibu na mpaka wa Kenya na Somali imeongezeka kwa zaidi ya thuluthi moja katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kambi hiyo kwa sasa ni hifadhi ya zaidi ya wakimbizi nusu milioni.

Mwaka jana , maelfu ya Wasomali walimiminika katika kambi hiyo kutokana na hali ya ukame, njaa pamoja na vita viliovyokuwa vikiathiri nchi yao.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Dunia Mike Wooldridge anasema kwamba wakati huu bado maelfu ya wakimbizi wanaishi katika vyandarua ambavyo vinazidi kuchakaa na kuharibika kutokan na hali mbaya ya ya anga.

Image caption Kambi ya Dadaab iko mpaka wa Kenya na Somalia

Mashirika hayo ya kutoa misaada inasema wakimbi wapatao 30,000 wanahitaji makao lakini kwa wakati huu kuna pesa za kusaidia wakimbizi 4,000 peke yake.

Maji safi kwa wakimbizi karibu 50,000 pia yanahitajika kwa haraka ili kuzuia wasipate maradhi ambukizi kama vile kipindupindu.

Wakati huo huo mashirika hayo yamesema kuna haja ya suluhisho la kudumu kutafutwa.