Uingereza yakiri dhulma dhidi ya Mau Mau

Image caption Mashujaa wa Mau Mau wakidai kudhulumiwa na uliokuwa Ukoloni wa Uingereza

Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Serikali ya Uingereza imekiri kwamba uliokua ukoloni wa Uingereza nchini Kenya ulitekeleza dhuluma za kibinadamu dhidi ya raia waliozuiliwa katika kambi zilizotengwa kuwaadhibu wanachama wa vugu vugu la Mau Mau ambalo liliendesha harakati za kudai uhuru wa Kenya.

Dhuluma hizi zilifanyika baada ya kutangazwa hali ya hatari nchini Kenya mwaka wa 1952.

Hatua ya sasa inafuatia ombi la mashujaa wa uhuru wa Kenya ambao wanataka mahakama kuu ya Uingereza kuamua ikiwa wana haki ya kufungua kesi dhidi ya serikali kutokana na dhuluma zilizotekelezwa na ukoloni huo.

Wapiganaji hao wa zamani wanadai kupata madhara makubwa wakati wa harakati hizo, wakisema mbele ya Mahakama Kuu ya Uingereza kuwa waliteswa.

Wanasheria wa wapiganaji hao wa zamani wa Mau Mau wanasema hii ni mara ya kwanza serikali ya Uingereza kukiri madai hayo.

Wakili wa serikali ya Uingereza, Guy Mansfield, amesema asingependa kupinga kwamba raia waliteswa na kufanyiwa madhila mengine wakati wa utawala wa kikoloni.

Hata hivyo serikali ya Uingereza inateta kuwa muda mwingi umepita na kwamba ikiwa kesi itafungulkiwa huenda kesi ikasikilizwa katika mazingira yasiyo ya haki.

Mnamo mwaka 2011, wakili wa mahakama kuu aliamua kuwa waathiriwa hao, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara wana hjoja nzitro ambayo lazima isikilizwe.

Mwakili wao wanadi kuwa bwana Nzili alihasiwa , huku bwana Nyingi akicahapwa vibayabwakati huku Bi Mara akibakwa katiak tukio baya zaidi la udahalilishaji wa kingono wakati wakizuiliwa katika kambi.

Mwathirika wa nne Ndiku Mutwiwa Mutua, tayari amefariki. Kifo chake kilitokea katika kipindi ambacho mahakama iliamua kuwa kesi yao ingeweza kuendelewa.

Kwa usaidizi wa wakalimani katika mahakama kuu, watatu hao wenye kati ya umri wa miaka 70 na 80, walihojiwa kwa muda mfupi, kuhusu ushahidi wao.

"katika miaka ya kabla ya uhuru wa Kenya,. Watu walichapwa , ardhi yao ikaibiwa na wanawake wakabakwa huku wanaume wakihasiwa pamoja na watoto wao kuuliwa" alisema Wambugu Wa Nyingi Kenyan Mau Mau claimant

Katika taarifa yao yanye kurasa 20, bwana Nzili, mwenye umri wa miaka 85,alitoa maelezo kuhusu namna alivyonyanyaswa na kuvuliwa nguo , kufungwa mnyororo na kisha akahasiwa kwa koleo kubwa ambazo hutumiwa kuhasi ng'ombe katika kambi moja ya wafungwa mtaa wa Embakasi viungani mwa Nairobi.

"nilihisi kuachwa bila matumaini yoyote. Sijawahi kupata watoto na sitawahi kupata hata mtoto mmoja.Pia siwezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkwe wangu alisema Nzili"

Bi Mara, naye mwenye umri wa miaka 73, alitoa ushahidi wake kuonyesha ambavyo alifanyiwa alipokuwa na umri wa miaka 15, alipelekwa katika kambi ya wafungwa ya Gatithi ambako alichapwa na waingereza na kisha kudhulumiwa kingono kwa kutumia chupa ya maji moto.

Alisema kuwa alihisi kudhulumiwa vibaya sana na kuachwa na uchungu mkubwa na kuwa uhuchungu huo umezidi na umri wake.

"Sielewi kwa nini nilifanyiwa hivyo kwa sababu tu ya kuwapelekea Mau Mau chakula." alihoji bi Mara.