Idadi ya waliofariki Zanzibar yazidi 30

Miili ya watu walioangamia baada ya feriu kuzama Zanzibar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Miili ya watu walioangamia baada ya feriu kuzama Zanzibar

Takriban watu 30 wamefariki dunia baada ya meli iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya mia mbili na hamsini kuzama karibu karibu na kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania .

Kwa mujibu wa taarifa zilizitolewa na kikosi cha wanamaji, watu wengine wengi wanaripotiwa kuokolewa kufuatia meli hiyo kuzama kutokana na dhoruba kali.

Mmoja wa watu waliofika katika eneo kulikotokea ajali hiyo na kushiriki katiia uokoaji ni Mohammed Omar ambaye aliambia BBC kuwa meli hiyo ilikuwa imepinduka na injini zake zikiwa juu: "wengi wa waliookoka ni wale wanaojua kuogolea vivi hivi na Mwenyezi Mungu."

Mwandishi wetu wa Dar Es Salaam, Hassan Mhelela, ambaye amekuwa akifuatilia ajali hiyo tangu itokee jana amesema shughuli za uokoaji zimeripotiwa kuanza tena.

Alisema zilisimamishwa jana usiku kwa sababu ya hali mbaya ya bahari na giza.

Mwaka mmoja haujakamilika tangu kutokea ajali nyingine kutoka katika njia hiyohiyo ya meli na kusababisha vifo vya mamia ya watu.