Ugiriki yatamani mkopo wa pili

Image caption Bunge la Ugiriki

Rais wa tume ya jumuia ya ulaya Jose Manuel Barroso yuko nchini ugiriki kwa ziara yake ya kwanza katika kipindi cha mika mitatu.

Wachunguzi kutoka jumuia ya ulaya na shirika la fedha duniani IMF wapo hapa kuona iwapo ugiriki imetimiza masharti ilowekewa kabla ya kupewa mkopo wa pili wa ufufuzi wa uchumi.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema patakuwa na ujumbe wa kuunga mkono kutoka kwa umma lakini malumbano makali yatashuhudiwa katika kikao cha faragha kati ya maafisa hao na serikali ya ugirki kuhusiana na masharti hayo.