Michezo ya Olimpiki yaanza hasa

Mashindano mbali mbali yaanza hasa Jumamosi katika michezo ya Olimpiki mjini London.

Moja ya michezo hiyo ni mashindano ya mbio za wanaume za baiskeli, lakini piya kuna gymnastics, kuogelea na basketboli.

Watu zaidi ya 15,000 walijitolea na kushiriki kwenye tamasha ya ufunguzi wa michezo Ijumaa usiku - tamasha la fakhari la mchanganyiko wa watu, tamthilia na muziki.

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, Jacques Rogge, alisema sherehe hiyo ya ufunguzi ilionesha yote yaliyo mazuri katika ubunifu wa Uingereza.