Mazungumzo ya kudhibiti silaha yakwama

Serikali ya Uingereza inasema kuwa imevunjika moyo kuwa mazungumzo ya kimataifa mjini New York yameshindwa kufikia makubaliano ya kudhibiti biashara ya silaha duniani.

Haki miliki ya picha Associated Press

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Uingereza, William Hague, alisema Uingereza haikufurahi na matokeo hayo.

Bwana Hague alisema, anatumai hatua kubwa imepigwa, na muda zaidi unahitajika kupata makubaliano ya wengi.

Mazungumzo hayo yalipangwa kufikia makubaliano jana, lakini yalishindwa kwa sababu Marekani, Urusi na Uchina zimesema bado zinazingatia maswala hayo.