Mashambulio ya Aleppo ni ya kusita-sita

Wanajeshi wa serikali ya Syria wameendelea na mashambulio yao dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji katika mji wa Aleppo.

Haki miliki ya picha AFP

Inaarifiwa kuwa watu zaidi ya 30 wameuwawa.

Lakini inaonesha jeshi la ardhini la Syria halijaweza kusonga mbele katika baadhi ya mitaa, na mwandishi wa BBC anasema, inaonesha vita vya Aleppo kwa sasa ni vya mashambulio ya mizinga na mabomu kila baada ya muda.

Katika eneo la Deir ez-Zor, wanaharakati walisema watu 17 waliuwawa wakati vifaru vilivopiga basi ambalo lilikuwa na watu waliokuwa wakikimbia mapigano.